Skip to main content

Uchungu wa Kuzaa + Kujizuia usi-Push = Near Death

Mimba ya mwanangu ya Pili Iman haikuwa enjoyable + alipitiliza. Mkunga kanaipangia siku ya kuwa "induced" ili nipate Uchungu.



Binafsi sipendi vitu ambavyo sio asili kwenye mwili wangu na hakika sio Uchungu, pia ni Mpinzani wa kuzaa kwa. C-section.



Kwabahati nzuri (Mungu alijibu maombi) Asubuhi ya kuwa induced "chupa" imepasuka, nikawapigia simu wakunga wakasema wanajiandaa kunipokea wakati wowote.



Mimi being mimi, nikasema nitavumilia mpaka maumivu yachanganye ili nikifika tu Hospitali nijifungue....maana kwa Barack ushamba/kutokujua tulienda Hospitali mapema....uchungu ukachanganya Saa saba....Lol!



Anyway, nikapata uzoefu mpya sasa....kama unadhani Uchungu wa Kuzaa ni kamambe!!....Usiombe Kuumwa uchungu huo + juhudi za kuzuia mtoto asitoke.




Mambo yakaenda vizuri, Uchungu unakuja unarudi....ikafika saa Kumi na mbili Jioni, mara booom! Mtoto namhisi huyu hapa....naita baba mtu, kusanya Barack....hao garini.




Najisemea "Mungu nisaidie mtoto asitoke" nikawa naumwa huku nazuia kusukuma....



Tumefika Hospitali Mume wangu akawapigia simu kuwa tupo Chini na sijiwezi, wakasema wanakuja na Wheelchair....



Aaaah ile nawaona tu kwenye Korido na mavifaa ya kuzalishia mwanamke nikajiachia....wananiambia "breath-breath aaah" nikawaambia "Iman is here".



Katikati ya Korido, mbele ya Mgahawa wa Hospitali Madaktari wanapata Dinner....Wakunga wakanilaza chini, madaktari wakaacha Dinner wakaja mbio kusaidia na kuweka "uwigo" for my privacy....one push Iman huyu hapa.




Wakakaweka kifuani then nikaletewa Machela (is it) anyway...wakakachukua na kwenda kukapa "first checks" in which kakafaulu 10/10.




Tukapelekwa kwenye Suite yangu ambayo ndio nilipaswa kujifungulia....Lol!




Misukosuko during my pregnancy....Iman is very special girl kwangu. Mwaka umepita, kananipa tantrums za kutosha.....naangalia nyuma....nacheka tu.


Kwaheri kwa sasa.....
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao