....imekuwa kawaida kwa Wanandoa Wake kwa Wame kutafuta "jinsi ya" kufanya mambo mbali mbali ili kuifanya Ndoa kusimama Imara na kuepusha misuko-suko ya kihisia na hivyo kupelekea Ndoa kuwa Ndoano na pengine kuharibika.
Hii kuwa "chini ya Mumeo" hata mie siijui na vyovyote ilivyo kamwe sitokubali kuwa "Chini" ya Mtu yeyote achilia mbali Mwanaume ila nitakuambia ninachokijua ambacho huenda ni tofauti lakini bado kinamrudishia Mwanaume hali ya kujihisi/sikia kuwa anaheshimika/heshimiwa na Mkwe.
Tatizo kubwa linalofanya Wanawake kukumbushwa au lazimishwa na Jamii kuwa ni LAZIMA wawe chini ya Wanaume (asiwe na Sauti) pale wanapoamua kufunga Ndoa ni kutokana na Imani kuwa Mwanamke anaposimama na "kujitetea" na/au kum-challenge Mwanaume basi huesabika kuwa hana Adabu, hana Heshima kwa Mwanaume husika.
Ukweli ni kuwa unapokuwa kwenye Ndoa ya "ndio Bwana" kwamba kila anachokisema Mwanaume wewe unakubali tu....huondoa Changamoto na hivyo kufanya Ndoa kuwa a bit "boring" na ni wazi kuwa hautofurahia Ndoa hiyo kwa sababu hautokuwa na Sauti,...Ndoa inaendeshwa na Mtu mmoja, kwamba kuna maamuzi yatakuwa yakifanywa na Mumeo ambayo wewe hupendezwi nayo lakini kwa sababu ya "Uoga" aka kuwa Chini yake ambako wewe unadhani ni "heshima" unaendelea kuwepo humo.
Ikiwa unatoa "Heshima" huku unahasira au Moyo/Roho inakuuma ujue hiyo sio Heshima bali ni "Uoga" ambao ukiendelea utakusababishia Matatizo ya Kiakili na Kisaikolojia(bila wewe mwenyewe kujua), utaishi kwenye Ndoa kwa sababu ya kufurahisha Jamii/Famili/Ukoo na sio kwa ajili yako na Mumeo na pengine Watoto kama mtaajiliwa.
Huenda ukawa unamalizia "machungu" yako kwa...labda Msaidizi wako,Marafiki zako au Watoto. Unaweza kuwa mwenye hasira kwa watu wengine ambao hawahusiki.....unatoa Sauti/unakuwa juu huko kwasababu huwezi kufanya hivyo kwa Mumeo. Hivyo unaumiza watu wengine wasio na hatia kwa Upumbavu wako wa kuwa Chini ya Mumeo kama sehemu ya Kumheshimu!!
Ndoa ni Muungano wa Watu Wawili, Wewe na Mumeo. Msingi wa Ndoa yenu unatakiwa kuwa-based na kuendelea kujengwa na pande zote....baadhi ya Mafunzo kutoka kwenye Imani za Dini yamepitwa na Wakati, ni vema kutumia Common Sense rather than kufuata "Mafunzo" ambayo ni Radical na zimeegemea kwenye Mfumo Dume zaidi na kutokana na Maisha yalivyo sasa ni kama vile baadhi hazileti maana? Kwamba tunakabiliana na changamoto tofauti na zile za Miaka 2000BC.
Sasa Heshima kwa Mwanaume ndio sababu kuu/pekee ambayo husababisha Wanawake waambiwe/lazimishwe kuwa Chini ya Mwanaume. Kama nilivyokusia hapo juu, Kuheshimiwa kwa Mwanaume ni Muhimu sana kama ilivyo kwetu Wanawake kwenye kujaaliwa,kulindwa na kupendwa (kuwa cherished).
Nnachojaribu kusema hapa ni kuwa, huitaji kuwa Chini ya Mwanaume! akifanya ujinga muweke sawa ila sio kwa Kumfokea bali kuwa-firm.....kwamba aone kuwa unachosema hutanii na hutaki mchezo...upo very serious.
Chagua Maneno ya kutumia, ikiwa unahitaji muda kufikiria, jipe muda na tafuta nafasi uwakilishe Issue inayokusumbua. Ikitokea kitu na kinahitaji mabishano basi Bishana kwa heshima bila kutoka nje ya Mstari wa Heshima na kutumia maneno machafu/kashfa..
Mara nyingi Wanaume huchukia ikiwa wewe Mwanamke unaonekana "smarter" kwenye Mambishano yenu na ili kukunyamazisha hukimbilia kutumia Kashfa au maneno machafu yatakayokuumiza hisia, sasa hata kama yeye atayatumia bado huitaji kumrudishia hapo kwa hapo. Ugomvi ukiisha/poa muelezee hisia zako za kutokupendezwa na matumizi ya maneno Machafu/Mabaya/Matusi.
Kuwa Chini ya Mtu yeyote sio rahisi, achilia mbali Mumeo, mie binafsi siwezi na sitokaa niweze na Yaye Mume wangu analijua hilo....sitaki/sipendi ujinga(naturally mie ni Mkali), nina hoji kwenye kila jambo/kila kitu ambacho kinagusa Familia yetu na hasa Watoto wetu....nadhani hii ni kutokana na sehemu ya "career" niliyopitia? sijui!!
Ndoa ni Kazi ya kila Dakika, Kila saa na Kila Siku, ukiwa mvivu basi utakimbilia "mwanamke lazma awe chini ya Mumewe"....acha Uvivu, do your Job! Kama huna Muda wa kufanyia kazi basi usifunge Ndoa....Ndoa haihitaji wavivu.
Usikose Post ijayo ya "Jinsi" ya kuonyesha Heshima kwa Mumeo. Nathamini na Kuheshimu Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai!
Comments