Skip to main content

Pale Mwenza wako anapobadilishwa tabia na "Rafiki"...


...Mara nyingi watu husema au kuamini kuwa Mtu anapopata Pesa au Kazi mpya inayolipa Vizuri kuliko kazi yake ya Awali huwa anabadilika(nadhani niliwahi kuzungumzia kwanini watu huwa hivyo mwaka jana/juzi). Habari? natumai Uumzima wa Afya.



Nirahisi kutodhani kuwa Mtu Mzima hawezi kuwa "influenced" na Mtu au Watu wapya wanaomzunguuka....kwasababu amepita Umri wa miaka 30...lakini kihalisia bado wapo Watu Wazima ambao wamekua Miili tu na Namba zimeongezeka lakini Akili zao bado ni za Kitoto. Bado wanapata hitaji la  kutaka kufanana, ku-fit in, kuwa kama yule/huyu,kukubalika n.k.


Inasemekana hali hiyo  hutokana na Ukosefu fulani wa "attention" kutoka kwa Walezi/Wazazi kipindi ambacho Mhusika alikuwa chini ya Miaka 10. Kumbuka matokeo ya Malezi  tuliyopata kutoka kwa Wazazi/Walezi wetu  huwa yanaathiri maamuzi (mabaya/mazuri) na Maisha yetu ukubwani. Mtu anahitaji kitu kidogo tu ku-triger alichokosa Utotoni. Achana na hili.



Sasa kwa baadhi mabadiliko huwa Wazi  mara tu wanapoanza "Shughuli mpya" hivyo ni rahisi kumuweka Mwenzio sawa na hivyo unakuwa umemsaidia kugundua "mapungufu" yake ambayo yanaathiri Uhusiano/Ndoa yenu.



Wakati mwingine inakuwa ngumu kugundua tofauti (hasa kwa Wanawake) kutokana na  Uchovu wa Shughuli zisizoisha za Nyumbani na Malezi ya watoto. Uchovu huo unaweza kukufanya ujishtukie na hata kujibebesha mzigo wa Lawama kuwa wewe ndio sababu ya mabadiliko ya Mwenza wako.



Utakuwa na bahati sana ikiwa Mwaka umepita tangu apate Kazi Mpya/Cheo/Mshahara Mzuri na Mwenza wako hajakutamkia kuwa "umebadilika sana", Jirekebishe, "Humueshimu", "hukuwa hivi siku za nyuma" bla-bla-bla. Sasa leo nitakupa au kukusaidia kuweza kugundua kuwa Mwenza wako aliepata Kazi Mpya au kupanda Cheo na Mwenye Mshahara Mzuri sio yule uliemjua tangu apate kazi Mpya au kupandishwa Cheo.


1)-Ukilalamika kuwa "leo umechoka", yeye atakuambia umefanya nini siku nzima? badala ya kukupa pole na ku-offer msaada au Massage. Kana kwamba shughuli uliyonayo sio muhimu na haichoshi kama yake. Hivyo ni yeye tu ndio anapaswa kuchoka. Na siku akilalama kachoka basi atategemea umfanyie kila kitu kama Binti/Bwana Mfalme.


2)-Anakuwa Mkosoaji kwenye kila jambo unalofanya/taka kufanya au anatoa Jibu ambalo sio "Possitive" kabla hujamaliza kusema/uliza ulichotaka kusema/uliza.


3)-Anapokuwa na siku za Mapumziko anatumia Muda wake huo kuongea na Rafiki zake badala ya kukusaidia vijishughuli viwli vitatu vya Malezi ya Watoto wenu(kama mnao). Kucheza na watoto sio Malezi...tambua hilo.


4)-Kila mnapofanya mazungumzo kuhusu Familia yenu lazima atachomeka Jina la Mtu wake ambe ndiye anam-influence na familia yake. Utasikia "hata fulani hivi, alifanya vile, anafanya hivi" n.k.


5)-Ukihitaji afanye/toe Uamuzi wa kufanya jambo fulani Muhimu kwa Familia yenu basi ataambia Usubiri/umuachie yeye kwanza afanye uchunguzi(anaenda kuwakilisha kwa Mtu wake anaem-influence).


6)-Akipatwa na Tatizo mbali na Nyumbani mtu wa kwanza kujua ni yule anaem-influence na sio Watu wa Msaada au Polisi na wewe Mke/Mume mtu ndio sahau...utasimuliwa tu.


7)-Zile Simu za Mara x2 kuangalia Watoto wameshindaje hazipigwi tena, Muda wote unamalizwa na huyo mtu wake anaem-influence.


Je! Ufanye nini ikiwa umegundua kuwa Mumeo/Mkeo "amebadilika" kutokanana kuwa-influenced na Mtu  baada ya kupata Kazi Mpya/Pandishwa Cheo? Usikose Post Ijayo.


Nathanimi na kuheshimu muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao