Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2015

Ujidhaniavyo sivyo....

Heiyaaa. Mara zote huwa tunaamini tupo vile ambavyo hatupo. Nitakupa mfano:-  Unapoenda kununua Foundation(matope ya kupaka Usoni kabla ya mengineyo) unachagua rangi ambayo sio yako na huwa waaaay lighter. Sio kwamba unakusudia bali hutaki kukubali ile yako ambayo pengine inaonekana ni nyeusi sana kwenye Chupa kuliko unavyoamini(kithihitisho ni Picha zako). Enzi nilikuwa na "Wifi" wa Kiarabu na kwenye familia yao kulikuwa na waliozaliwa nje ya "uarabu" kwamba mzazi mmoja alikuwa Muarabu mwingine Mweusi halafu mtoto (binti) katokea mweusiiii mwenye nywele za kiarabu. Basi tukijikusanya tumapiga stori huyo binti alikuwa anapenda kuwasema wadada wengine kuwa ni Weusi mno kiasi kwamba hawavutii. Kwasababu mzazi wake mmoja ni Muarabu na anaishi kwenye Familia Kiarabu aliamini kuwa na yeye ni Muarabu. Hiyo pia huwatokea watoto waliochanganya na Wazungu na kuishi Uzunguni zaidi kuliko Weusini...huwa wanajidhania kuwa ni Wazungu(rangi wise). Kingine ni uwingi wa nywel

Magaidi wa Kiislam...

Ahsante kwa kuichagua Blog hii.....natumaini umeanza Wiki yako vama. Post ya jana inaweza kukufanya udhanie kuwa naunga mkono Mauaji ya hao Waislamu(if you are that thick). Ukweli ni kuwa tangu 7/7 London Bombing sina Imani wala huruma na Waislam wa UK. Victoria line au Piccadilly ndio lines zangu then nateremkanpale KingX......siku hiyo ya Saba-saba niliamua kutega Kipindi cha asubuhi kilichokuwa kinaanza saa 9:30am.....ningetoka muda wangu wa kawaida labda leo nisingekuwa hapa. Nilipoona Waislamu nahofia kuwa wanaeza jilipua.....miezi michache ya 2005 baada ya 7/7 nilikuwa nahama behewa(kwenye Tube) su nasubiri the next one ikiwa kuna mkimama au mkibaba alievaa Kiislam au mwenye asili ya Waislam kama vile Wasomali, Wapakistan n.k. Mpaka leo karibu miaka 10 naishi masaa 8 driving kutoka London na Dakika 45 kwa ndege (Dar to Moshi....pata picha)bado naogopa kujimix na hao majamaa(wapo kila kona). Baada ya kilichotokea Tunisia hakika kinaongeza hofu na chuki inakua dhidi ya Waisla

Usilaumu kabla hujajua kwanini

Aah kuumwa aka holiday(mpaka niumwe ndio napumzika kuwa Mama a little).......jikapata nafasi ya kusoma article moja (ndefu ka kitabu)kuhusu Wabritishi wanaojiunga na ISis. Nimepata mwanga mpya kuhusu hao jamaa na yote wayafanyayo. Imeeleza kwa kifupi tu kuwa Kuishi Nchi za Kimagharibi kunawafanya wajihisi kuwa sio Waislam enough. Ukifuatilia hnagundua kuwa ni kweli kwasababu  Muislam wa kweli hawezi kuishi Nchi kama Uingereza.....wanaoishi humo ni wale wanaotaka kuubadilisha Uislamu ili kwenda na wakati, kwamba wanataka kuwa Waislamu wa kisasa. Vijana hao wanadai kuwa Wamekuzwa Kiislamu na Wazazo wao lakini baada ya kuwa watu wazima wamegundua kuwa Wazazi wao wamekosea kwa kuja kuishi Uingereza. Kuishi Uingereza kunamfanya Muislamu kutokuwa Muislamu kwasababu ya Mazingira, Utamaduni,Ubaguzi na kufunga Masaa 19 mwezi wa Ramadhani(nimeongezea hihihi). Mpaka leo sielewi ni kwanini hasa Waislamu hukimbilia Nchi za Kimagharibi(za Makafiri) na kuacha Nchi za Kiislamu tulivu? Au kama wa

Utumiaji wa Anti- wrinke....

Unashangaa Kijana wa miaka 20na anatumia Cream za mikunjo usoni kuna tofauti gani na wewe(mie) unaetumia za Mature people wakati hata hujafika miaka 40? Za umri chini ya miaka 60 zinanipa vyunusi bana na nyingine kukausha ngozi kupita kiasi......nilipojaribu za mature people(miaka 60+) sikupata vyunusi na ngozi ikawa na afya njema. Sio mbaya kuanza mapema kuitunza ngozi yako kwasababu anti-wrinkle actually haziondoi wrinkle(mistari/mikunjo usoni) ila inachelewesha sio? Sasa kutokana na masitiresi ya maisha bana watu wanapata Mikunjo kabla ya umri. Makampuni ya utunzaji wa Ngozi nayo yanakategolaizi antirinkozi kuanzia miaka 25(well wenzetu Weupe wanakunjika mapema so yeah). Kwa kawaida Waafrika(Weusi) huwa hatupati makunyanzi mapema na wengi wetu huwa tunaonekana wadogo kuliko Umri wetu. Aaah! Stori time*** Siku nipo kwa Dentist akaja madada na Pram yake....anaulizwa utambulisho wake (jina na DoB) akageuka kuangalia nani anatilia maanani....akamnong'oneza tarehe akamalizia na

Mwili ni Mashine....

......inayo-process Kemikali (chakula na mengineyo)....kuna wakati Machine inahitaji "huduma" ili kuendelea ku-process Chemicals ili uendelee kuwepo. Njia pekee ya wewe kujua kuwa Mwili(Mashine) inahitaji " huduma" no mwili huo kukuambia kwa ama kuumwa au kujisikia ovyo/vibaya. Hapa sizungumzii kuumwa Magonjwa ya kuambukizwa na Mbu au Virusi (Mafua, Tetekuwanga au hata HIV)au yale ya kurithi kama Moyo, Kisukari n.k. Kuna watu ambao wanaishi wakitegemea Dawa kusaidia Mashine zao kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu.....kwamba mwili unaposema "mamaa nimechoka nahitaji kupumzika"....mwenye mwili ana pop a Chidonge au Mavidonge. Celebs wanakuambia ili ufanikiwe unatakiwa kufanya kazi bila kuchoka (wana pop pills hao).....katika hali halisi mtu huwezi kusafiri kila siku na kufanya shows usichoke! Huwezi ku-pop pills kila siku za maisha yako kwasababu unaongeza Chemicals mwilini na hivyo mwili kufanya kazi ya ziada na hivyo ku-over choka. Nachukua a year o

Bahili, Mchoyo au Mbinafsi...

Heeiyaaa! Shukurani kwa uwepo wako siku ya leo. Watu wa hivyo tunaishi nao lakini kwasababu tunawapenda(Mapenzi upofu) inakuwa ngumu kujua au kutambua. Hawa bwana wanaweza kukufanya uishi maisha ya kiupweke kabisa na huzuni na hivyo kuondoa maana ya Umoja wenu. Sasa leo nataka ujue kiduchu tu. Wale majaa wanaotaka kujua umetumiaje Pesa na wakigundua umetumia senti kwa matumizi yako binafsi ambayo wao (wanaume) wanaamini kuwa sio muhimu wanaanza kung'aka! Wakati mwingine unaona unaongeza mavazi ya watoto ili wapendeze lakini bado mtu anakuambia "mbona wanakila kitu"....Inafikia mahali unaanza kuhisi kama vile unasimangwa na hivyo unaamua kutumia pesa zako. Akiona Pesa anazotoa zinatumika kwa kile anachodhani au kuamini kuwa ni "muhimu" lakini bado unapendeza na watoto wanapata vitu vipya na vizuri mara kwa mara anaacha kutoa Pesa za Matumizi.....huyu ni Bahili! Mchoyo; Mara zote akirudi nyumbani baada ya Kazi....unamuandalia chakula  anakuambia "nilipi

Maisha ya sasa ni kusaidiana...

When it suits them.... Sina uhakika na wenzetu wa Nyumbani ila wengi wetu wa Ughaibuni (wanawake) tunalaliwa na Wanaume tunaoishi nao aka Wenza/Waume. Maisha ya Ughaibuni ni Magumu sana japokuwa upatikanaji wa vitu basic ni rahisi.....kwamba huwezi kuvaa nguo/viatu vilevile au kutumia Friji/Jiko/Kochi lilelile kwa miaka mitatu. Lazima kutakuwa na hitaji la kununua vipya(ni kwasababu ubora wake ni wa chini) lengo la Makampuni mengi nikuwawezesha Wananchi "wa kawaida" kumudu vitu ambavyo vinafanya maisha yao kuwa rahisi(kurahisisha maisha). Au tuseme ni "kiwango cha ubora wa maisha" kwa kila mwananchi kilichowekwa na Serikali.......sasa ukiamua kuibuka na Sumsang Fridge sababu unamudu hakika utakuwa nayo kwa miaka 10 zaidi. Turudi kwenye Kichwa cha Habari; Ughaibuni sote tunafanya kazi (mimi bado ni Temp Mama wa kunyumba)na tuna-share majukumu Kiuchumi  lakini linapokuja suala la majukumu ya kuangalia/kulea watoto tunaambia ni "jukumu la mama". Kwamba

Aah namjua yule....

Hello! Ishi ujifunze au kua uyaone.....kuna wale jamaa(wake kwa waume) huwa wana uzoefu wa kila jambo linalotokea Duniani. Au wao wanamjua kila mhusika anaepatwa na jambo lolote interesting kwa ubaya au wema. Sijui kuhusu wewe ila mie huwa wananiudhi sana! Unaweza ibuka unazungumzia habari ya kushtusha kuhusu mtu fulani baada ya kusikia Taarifa ya Habari then "msikilizaji wako" anaanza kukupa historia nzima ya mtu huyo na matokeo yote maishani mwake. Unamuuliza umejuaje yote hayo mwenzangu? anakuambia "aah niliwa kuishi nae mtaa mmoja" au "mama yake alikuwa mpangaji wetu" nakadhalika! Haiwezekani umjue kila mtu kwa undani (dont you have life?)lakini inawezekana unajua habari za kila mtu au watu wengi kwasababu ya Umbea au kwasababu unafuatilia sana habari za Kidaku. Wakati mwingine wewe sio mbea lakini marafiki zako ni wafuatiliaji wazuri wa habari za watu na kukupa "stori".....sasa wewe kujua stori za watu haona maana kuwa unawajua sema un

Wanawake na Usenge!

Kwanini sisi wakimama ni wepesi sana kukubali hawa jamaa?.....Hi are you well? Usinielewe vibaya! Siwachukii wanaojibadilisha kutoka Jinsia moja kwenda nyingine(I feel sorry kwa mume/mke na watoto though). Pia sina habari na Wanaume wanaopenda kujiremba au kuvaa nguo za kike. Hakika sijali nini mwanaume na mwanaume mwenzie au mwanamke na mwanamke mwezie wanafanya chumbani kwao(keep it there). Lakini sitoacha kujiuliza au kuuliza ni nini hasa kinafanya wanawake kuwa wepesi kuwakubali hawa jamaa kwenye Jamii? Kwanini sisi ni wa kwanza kuwachukulia poa na hata kurafikiana nao? Ni ile "huruma nature" tulioumbwa nayo au ni kwasababu Wanaume wengi ni Waoga wakidhani hali hiyo(Usenge) inaambukiza so wanakuwa wagumu au wenye Chiki/hasira wakihofia "kubadilishwa"? Pengine wanaogopa kuwadondokea Wasenge wa Kiume hihihihihi kama unaeza mtamani wa jinsia yako akiwa Mtupu na ukawimika wewe ni Msenge tu hata kama umeoa na unawatoto.....usiogope toka Kabatini. Back to the po

Mashindano.....

Ni vema kuwa Mshindani mahali pa Kazi, Shuleni au Kimichezo, kwamba ni vema kuhakikisha unakuwa juu/mbele kuliko uwezo wako. Unaweza kuwa umezaliwa hivyo(mshindani) au umejifunza kutokana na "kusukumwa" na Wazazi wako. Nimewahi kuzungumzia hili lakini niliegemea zaidi ushindani kati yako na watu wengine uwaonao kwenye Sosho media au Mtaani(au was it in my head?). Pamoja na kuwa ushindani unakusaidia kufanya vema kwenye maisha yako Kikazi, Kielimu au Kimichezo bado hali ya Ushindani au kutaka kushindana pasipo husika kunaweza kukuharibia. Ukiiendekeza hali hiyo na kuiweka kwenye kila kitu ufanyacho inaweza kuumiza watu wako muhimu kama vile mke/mume, watoto na ndugu. Kabla ya kufanya mapenzi hii inakuna kichwani "juzi na jana nilianzisha mie au nilikuwa juu.....leo zamu yake. Bila kusema unamsukuma au kumvuta mwenzio awe juu yako"? Huo ni ushindani na can put mkeo/mumeo off. Katika hali halisi....anaelianzisha ndio atakae so huyo huyo ndio awe mtendaji mkuu, k