Skip to main content

Era ya Kulazimishana ku-react!


Heiyaaa!

Mtu una-react kutokana na Uzito au Wepesi wa Hisia  unazopata kutokana na Tukio au Jambo fulani. Kuguswa kwako kunaweza kutokana na Upendo au Chuki au Kutojali, Kutoona umuhimu wa jambo hilo lililotokea n.k.




Kama unakumbuka Rais aliyepita alikuwa mzuri sana/Maarufu kwenye kushiriki Masuala/Matukio ya Kijamii. Naamini kufanya kwake huko kulitokana zaidi na kuguswa kwake yeye kama Mwanadamu na sio kama Kiongozi wa Nchi. Kwamba anapojitokeza Mahali, haendi kuwakilisha Taifa basi yeye na pengine Familia yake. Reaction yake kwenye Misiba ilichukuliwa kivingine....achana na Siasa(Msimamo wangu kwa JK bado ni ule ule hihihihi), ni mfano wa karibu ili unielewe.




Sasa kwenye Era hii ya Sosho Media imekuwa ngumu na pengine haikubaliki kwa baadhi yetu kuweka wazi hisia zetu kwa kuhofia kuonekana "tuna roho mbaya", "hatujali", "tunachagua matukio yapi ya kusikitika/kufurahia", n.k.



Imefikia mahali wale "Magwiji" sijui "Wakongwe" (waliokuwemo kitambo kwenye Sosho Midia) kulazimishana ku-react na matokeo yake utakuta kila Blog/Site inazungumzia tukio lile lile kwa Siku kadhaa......kama ilivyo kwenye News Media. Sasa pengine Blog wanakimbiza "traffic" kwa sababu za kimapato zaidi na sio kwamba wanajali,umia au chukizwa  na tukio fulani lililotokea.




Platform kama Twita na Facebook zimekuwa zikitumika kulazimisha watu wa-react au ku-fit in na kuonekana(hata kama hawana hisia hizo) kuwa wameumia na wanajali kuhusu Tukio fulani linaloendelea kwa wakati huo.





Nitakupa Mfano mwingine. Linapotokea Shambulio au Maafa kwa Nchi kama India, Nigeria,Pakistan, Palestine, Ukrain, Russia na Israel huwa sipati hisia yeyote(nimechoka kusikitika na kukasirika), huwa si-react(nakuwa kawaida tu)....sasa silazimiki kuungana na wale walio-react kwa furaha au hasira au chuki na huruma......Hisia hailazimishwi, inajitokeza tu yenyewe.





Ikitokea umeguswa na tukio, usianze kuhamishia hasira zako kwa watu wengine na kuwalazimisha waungane na wewe au na ninyi ili "kuonyesha" kuguswa sawa wakati wanajua kabisa hawajakuswa kama ulivyoguswa wewe.





Imefikia mahali mtu unaamua ku-fit in ili uwe-protected na Magwiji uliowakuta kwenye hiyo Sosho Midia, kwamba ukienda tofauti na mtu na ukawa-attact maGwiji wanakuja kukusaidia. Umezoea ku-fit in mpaka unapoteza uwezo wa kujitetea. Ukiwa mtaani ana kwa ana na attacker au bully utafanya nini?





Labda tujaribu kuacha  Kacha ya kutaka  # zetu ku-trend kwenye Sosho Midia na hivyo ku-bully wenzetu ili wa-fit in na vile tunavyohisi sisi. Kila mtu ana haki ya kuweka/kutokuweka Hisia zake wazi, japo ni muhimu kuzingatia Sheria za unapoishi ikiwa unataka ku-share Hisia zako ambazoo ni Hasi. Tukubali kutofautiana iwe Kijinsia, Kiuchumi, Kihisia na mengineyo.



Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao