Skip to main content

Kulazimisha Mtoto awe na Mawazo....


Pengine ni ngumu kujua tofauti ya ku-share information kwa nia ya kuwafanya watambue "Asili" yao, wajifunze kuhusu Upande wa pili(kwa wale waishio Ughaibuni) na kuwapa watoto mawazo.




Natambua kuwa kila Mzazi ana namna yake ya kulea na kufunza wanae, na kamwe sitokufundisha namna ya kulea wanao tangu mie mwenyewe  najifunza kila siku. Lakini tukumbuke kuwa kuna "Common Sense".....huitaji Elimu wala Uzoefu kuitumia.



Unakumbuka ulipokuwa Mdogo na Mama au Baba au mtu yeyote wa karibu anaanza Hadithi za "Kaka/Dada" yako aliezaliwa na kufariki.....kisha ukaanza kuwaza ingekuwaje hivi sasa kama angekuwepo? Unawaza huko aliko je anafuraha, ana-toys,? unakuwa na Maswali kibao ambayo hayana Majibu. Mtoto anakosa usingizi kwa Mawazo au Uoga na akilala anamuota "dada/kaka". Wazazi hapa hudhani/amini kuwa Mtoto ana connection na "mwenzie"....lakini ukweli ni kuwa anasumbuka Kiakili na Kihisia.





Pia umewahi kutambulishwa kwa Ndugu yako ambae Baba/Mama alizaa wakati wa "ujana" na sasa anaishi na Mzazi mwingine ambae sio Baba/Mama yako. Unaanza kuwaza na ku-wish ama ungeishi kule au yeye angekuja kuishi hapo kwenu. Unatamani kuwa Wazazi wenu wangekuwa wamoja(baba na mama mmoja). Kwa Mzazi mmoja ambae ni Mzazi wa Mtoto wa Upande wa pili huona ni Jambo jema kwamba Mtoto huyu ana-value undugu wake na mtoto yule wa kabla ya Ndoa......Ukweli ni kuwa unateseka Kiakili na kihisia kuhusu Jambo hilo.




Halafu unakumbuka ile hofu uliyokuwa nayo pale Mzazi wako anapokuambia hana Pesa na XMas imekaribia, sio tu mtakula Ugali badala ya Pilau pia hakuna Sare  Mpya za Shule, Madaftari wala Kalamu....yaani unaenda shule na Sare zako zilizochakaa. Unapata Donge rohoni(unaijua ile hali ya kutaka kulia lakini huwezi kulia, huwa kuna maumivu  si maumivu fulani sehemu ya Koo hihihihihi)....Roho inakuuma na unakosa Amani kabisa kila Baba/Mama anaporudi Mikono Mitupu na ni tarehe 22 Dec!!....kwa Mfano.




Mzazi hapaswi kumuambia Mtoto kuwa hana Pesa, hilo ni jukumu lako kwasababu wewe ndio ulieamua "kumleta" ama kwa Uzembe au kwa Kupanga. Kwanini huamishie "Hatia" zako kwa mtoto na hivyo kumpa mawazo? Kama mzazi tafuta namna kwa uwezo wako wote  na kuhakikisha unatimiza mahitaji ya Mtoto. Mtoto haitaji kujua kama una Pesa ama huna au unazipataje.



Kuna wakati unakuta Mtoto anakuwa Mkimya sana(anakuwa na mawazo au depressed), lakini kutokana Umri wake unadhani kuwa hana Mawazo na hivyo ameamua tu kutulia leo(ameamua kuwa  mtoto Mzuri). Ukweli ni kuwa Mtoto anaanza kuwaza akiwa na Umri Mdogo sana kuliko tunavyofikiria.




Wazazi ndio chanzo cha Mengi Mabaya au Mazuri linapokuja suala la Ukuaji wa mtoto Kiafya, Kiakili, Kisaikolojia n.k. hivyo ni muhimu kutafakari na kujua Mipaka ya Info gani zinapaswa kuwa shared kwa umri husika.




Mtoto anapozaliwa huwa Mtupu akilini. Kila siku hujitahidi kujaribu na kufanya mengi, Mtoto huyu haitaji kuwa "feeded" masuala mengine ambayo hayamhusu kwa Umri alio nao! Muache mtoto awe mtoto.....muache awe huru. Mtoto anakabiliana na mengi katika kujifunza na hivyo haifai kuanza "kupandikiza" hatia zako za Mtoto uliemuacha kwa Baba/Mama yake, kwa mtoto huyu kwa kisingizio cha "nataka ajue kuwa ana Kaka/Dada" hai au katangulia.




Pia sio sahihi "kupandikiza" hatia za ukosaji wako wa pesa kwa mtoto kwa kisingizio cha "nataka ajue ugumu wa kutafuta" au "nataka ajifunze mapema kuhusu utafutaji wa Hela". Subiri mpaka afikishe Miaka 8, pale unapoanza kumshikisha Pocket money(pesa ya kutumia shule) tena unamfunza kutunza sio "kutafuta".



Wacha niishie hapa, Nathamini na Kuheshimu Muda wako hapa,  ahsante sana kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao