Skip to main content

Mzunguuko wa Ngono kwa Mwanamke...

Jambo!

Kama unakumbuka niliahidi kuwa nikipata muda nitaandika kuhusu Mzunguuko wa Hedhi ambao unaendana na Mzunguuko wa Kufanya Ngono/Mapenzi kwa Mwanamke. Nilielezea kuwa Mwanamke sio kama Mwanaume, kwamba tunakabiliana na mambo mengi ukiachilia mbali Homono(Pengine ni Homono tu).




Kuna siku Mwanamke analianzisha, inaweza kuwa mara moja au tatu kwa mwezi. Pia kuna siku mwanamke anataka kuwa Juu sio kwasababu wewe Mkibaba unataka bali mwili wake unamtuma kutaka kuwa in-control na hii inaweza kutokea mara kadhaa ndani ya mwezi lakini sio kila siku. Hali kadhalika zipo siku(ambazo ni nyingi) mwanamke anataka kuhisi kupendwa  na kujaaliwa kwa vitendo(kitandani)......vinginevyo Tendo halitokuwa na maana na halitokuwa la kufurahia.




Wale Wanawake na Wanaume mabingwa wa kuwalaumu wanawake kuwa ndio sababu ya Waume zao kutereza nje ni ama hawaujui Mwili wa Mwanamke, kwamba mwanaume ataka na kutegemea Mwanamke awe in control kila siku......au kungojea Mwanamke alianzishe ili afurahi au ajihisi Mfalme.



Tusipoteze  muda sana....twende kwenye Mzunguuko (Siku 28 ndio nina uzoefu nao).


Wiki ya Kwanza(Siku ya  1-7):  Siku unayoanza Hedhi/ona damu ndio Siku ya kwanza ya Hedhi na ndio unaanza Wiki yako pia. Haijalishi imeanza saa ngapi. Unakuwa umechangamka na utahisi Akili yako imetulia na kufanya kazi vema. Unapata "ari" ya kufanya mambo tofauti au mengi-mengi.Unakuwa kind too active.

Wiki hii ni nzuri ikiwa unaenda kwa siku 2-3. Wiki hii utahisi kutaka kufanyanyiwa Mapenzi zaidi ya wewe kuwa "mtendaji".




Wiki ya Pili(Siku ya 8-14): Wiki ya Kujiamini na kuhisi kutaka, unakuwa Muongeaji kuliko siku nyingine, unahisi kumpenda mwenza wako(au kutamani kupenda kama huna), unahisi kuwa na Nguvu nyingi na hujui hata uzitumie vipi!!



Hamu ya kutaka kufanya mapenzi huongezeka, unataka kuwa kwenye Control. Wiki hii Mwili wako "huchemka".....Vijana mnasema kuwa "hot", Ute wako unakuwa laini na uke "kulowa" kama vile upo tayari kwa Tendo. Wiki hii ndio Mwanamke unajiweka mwenyewe Juu, unakuwa mtendaji Mkuu na pengine kutotosheka na Tendo.Wiki hii pia ni Hatari ikiwa huna mapango wa kuwa Mama, hivyo kumbuka kutumia Kinga.




Wiki ya Tatu(Siku ya 15-22): Shughuli ya Uanamke ndio huonekana hapa, unakuwa na ama Huzuni au Hasira, msahaulifu, kila kitu unaona kero tu. Wiki hii hakuna Hamu ya kufanya mapenzi wala kufanyiwa Mapenzi. Mwenza wako asipokuchokoza na kwa kujituma kweli kweli kwenye "maandalizi" tendo linaweza likawa la maumivu/karaha. Pamoja na yote hayo bado Wikii nii salama, kwamba kama umehesabu vizuri basi huwezi kushika Mimba.




Wiki ya Nne(Siku ya 23-28); Siku Sita kabla ya kuingia Siku ya 28(siku yako ya Hedhi), utaanza Wiki hii kama ulivyokuwa Wiki ya Tatu, tofauti ni kuwa Wiki hii utakuwa na Nyege(hamu ya kutaka kufanya mapenzi) nyingi. Utakuwa Mkali na mwenye Kisilani labda.....lakini ukiguswa Kiuno tu tayari "umelegea".



Ikiwa Mumeo anajua Mzunguuko wako hapa ndio huwa anakutegea.....unamjibu kwa kiburi, yeye anakuja kukushika kwa nguvu na Kukubusu, halafu unakosa la kusema unaishia kupeleka Mkono kwenye nanilihu....hihihihi. Wiki hii ndio ile "sex when angry" huwa tamu. Umewahi kumtaka Mumeo aende kwa Kasi na Kwa nguvu? yeeah, basi lazma utakuwa unakaribia Hedhi aka upo Wiki ya Nne.



Hata hivyo, "hasira" nilizogusia hapa ni zele zetu wanawake kutokana na Homono, sio zile kuu na chafu. Hey Post imekuwa ndefu, wacha niishie hapa.


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao