Skip to main content

Kukosoa na Kumcheka mtu ni "interest" yako?

Nakuona!

Wengi huamini kuwa ukiwa na tabia ya kukosoa au kucheka watu wengine basi wewe utakuwa na Matatizo kwenye Maisha yako, maisha yakoo hayana furaha na yamejawa na Huzuni na hivyo kukosoa na kucheka watu ndio njia pekee ya kujipatia "furaha".



Nakubali kwa kiasi fulani, kwa baadhi kuwa Hasi kwenye kila kitu  ni tatizo na linaathiri maisha yao ya kila siku. wengine huamua kuwa Hasi kama sehemu ya kupata "attetion" au "Trafic" na "Views" popote walipo kwenye Sosho Midia.




Kwa wale wa Ughaibuni, Maisha mitaa hii yanaweza kuwa ya Upweke sana na hivyo kumfanya mtu kutumia muda wake mwingi kwenye kutafuta "furaha" kwa kuwa Negative towards watu wengine. Upweke wa huku unatokana na utofauti wa Kitamaduni, Utaratibu wa kazi za "shift",  Majira ya Mwaka(Kiza kuingia mapema) vilevile kutumia muda mwingi kusafiri to na from work....by the time unafika nyumbani upo hoi, tayari ni Giza hivyo  hakuna muda wa kutoka au kukaribisha watu kwako as kesho unatakiwa Kazini.




Nilipokuwa Teen nilijulikana kwa baadhi ya wanafunzi wenzangu kuwa "Dinah siku zote huwa na sababu ya kukosoa", nilikuwa na tabia ya kuchea watu, haijalishi  mtu kafanya nini jema lazma nitapata/ona Kasoro na kukosoa....by doing that wenzangu walikuwa wanacheka balaa!



Sasa, Darasa letu lilikuwa juu (Ghorofani) na hivyo tulikuwa na tabia ya "kuwachora" Wanafunzi na Wageni waliokuwa wanakatiza maeneo ya Nje ya Gate ay ndani ya Gate. Wakati mwingine nilikuwa busy na mambo mengine, lakini bado wataniita ili nione kasoro ya watu au mtu na hivyo wao kupata Burudani.



Ilifikia mahali nikachukulia kuwa kucheka watu ni "interest" yangu, kiukweli napenda kucheka na huwa najicheka mwenyewe.....lakini kucheka watu haikuwa sahihi. Mwaka 2010 ndio nikaamua kubadilika. Ni baada ya kushika Mimba.....Mimba ikanibadilisha. Nikatambua kuwa unapokosoa mtu ama watu kama sehemu ya "burudani" ni wazi kuwa unatatizo, sikuwa na sababu ya kukosoa na kucheka watu.



Unapomkosoa mtu kila siku hata kwa yale mema au yale yasiyohitaji "maoni" yako huko kunakuwa sio kukosoa tena bali ni kumchukia mtu huyo. Kwanini umchukie mwenzio/wenzio? wamekukosea nini? Pamoja na tabia hiyo  ya ajabu bado sikuwahi kucheka Walemavu, Wenye matatizo au Masikini zaidi yangu.




Era ya Sosho Media imewarahisishia wale watu ambao wapo kama nilivyokuwa mimi huko nyuma. Tofauti ni kuwa mimi nilikuwa nafanya hivyo bila kuwagusa wahusika moja kwa moja. So walikuwa hawajui nawakosoa kuhusu nini. Siku hizi mtu anakufuata live kwenye "profile" na kuanza kukukosoa.....anakuwa na utaratibu huo kila siku.



Mwaka 2013 niliugua PD(stori yake itakuja siku ingine)....baada ya kupona nikajifunza kuwa "Chanya" kwa Msaada wa Daktari. Hapa ndio nilipojifunza kuwa mambo mengi yanatokea kwenye Maisha ya mtu, huwa kuna sababu. Mpaka uijue sababu ya yeye kufanya alicho/anachokifanya ndio umkosoe. Kama hujui basi muache kama alivyo.




Kukosoa ni tofauti na Kujaji......bado najaji (siwezi kujizuia), pamoja na kuwa nitakujaji  bado sitokucheka. Heeey, ahsante kwa kuichagua Blog hii. Tambua nathamini na kuheshimu muda wako hapa.


Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao