Skip to main content

Kupoteza Nywele baada ya Kujifungua Update (Bidhaa)....

Natumaini Post hii itakukuta ukiwa Mzima wa afya.
Kama nilivyoahidi, leo nitakuelezea utaratibu wangu uliosababisha nywele(Relaxed) zangu kurudia Afya yake baada ya kuzipoteza na kupata "upara" wa muda.
Jikoni kuna mwanga asilia, sihifadhi Bidhaa hizi Jikoni....hihihi!




Ukiachilia mbali kuongeza aina ya Mboga iitwayo Kale kwenye Mlo wangu wa kila siku na kula Mayai 2-3 kila asubuhi. Bidhaa hizi zimechangia kwa kiasi kikubwa kuzuia Nywele zangu kuendelea kung'oka/anguka baada ya Kujifungua.



Utaratibu wangu Rahisi.

Kila Siku: Napaka Cantu Shea Butter kila siku asubuhi na Jioni na baada ya kupaka Cantu huwa na-"seal" na Mafuta asilia ya Sweet Almond.



Kila Wiki: Huosha na Deep Condition Nywele zangu mara Moja (kila Ijumaa/JumaMosi) na huwa natumia Cream of Nature shampoo. Baada ya hapo nafanya deep condition kwa kutumia Vitale Mayonaise ambayo huwa nachanganya na Hello hydration (haipo pichani) na aina 2 za Mafuta asilia ambayo ni  Nyoyo(Costor oil ) na Olive(extra virgin.). Huwa nakaa na mchanganyiko huo kwa Dakika 45-Saa Moja nikiwa kwenye Steamer.


Nasuuza kisha napaka Keracare Natural texures na Keracare normal leave ins na kisha kukausha nywele kwa kutumia Blow dryer(nitaweka Picha ya Tools kwenye post nyingine).



Kila  baada ya Mwezi: Naosha(deep clense/clarify) Nywele kuondoa uchafu uliosababishwa na bidhaa nilizokuwa natumia kwa mwezi husika na hapa huwa natumia Vitale Breeze Shampoo na kutumia Mchanganyiko wa Deep conditioner nitumiao Kila Wiki.


Kila baada ya  Mwezi na nusu: Huwa nafanya "Protein treatment" kwa kutumia Aphogee step 2(fuata maelekezo kwa makini) na baada ya hapo huwa natumia Keracare Humecto ili kuepusha ukavu/ugumu kwenye nywele.




Kila baada ya Miezi 3: Huwa nahina(kupaka Hina kwenye Nywele). Hina nitumiayo ni ile asilia moja kwa moja kutoka Mtini(naagiza kutoka Tanzania). Huwa nachanganya na Chai  ya joto kiasi, kisha naiacha kwa masaa 12 then naipaka na kuiacha kwenye Nywele kwa masaa 3 hadi 5.
Baada ya hapo naosha na kupaka Keracare Humecto conditioner ili Nywele zisiwe kavu/ngumu. Hina inaongea "nguvu"  kwenye nywele kama Protein  na pia huzilainisha ila mie naitumia kwa ajili ya Rangi kwani nywele zangu si Nyeusi vya kutosha  na sipendi Weusi wa kutosha  hihihihihi so yeah kale kawekundu ka Hina kanaweka u-brown-ish Nyweleni. 



Hakikisha kuna nafasi ya kutosha kati ya Protein treatment na Hina Treatment. Mie huwa naweka Relaxer kila baada ya wiki 10 na Miezi  Mitatu(Wiki 12) na wiki  mbili  au Tatu baadae ndio nafanya Hina treatment.


Kama hujawahi kujifungua na kupoteza nywele au Nywele sio muhimu kwako basi huwezi kujua umuhimu wa Post hii. Back then hakukuwa na Post nyingi online, nilihangaika mno kutafuta maelezo ya nini cha kufanya na namna ya kufanya (sikuwahi kupatwa na issue hii). Naweka uzoefu wangu ili Mwanamke mwingine mwenye tatizo hili asihangaike sana kama mimi. 


Ijumaa (Christmas day) hii nitanyoosha Nywele zangu na kuchukua picha na kulinganisha na ya 2014 ili niweze uweze kuona  tofauti na "upara" wangu wa muda.....hii itakuwa kwenye Post ya Vifaa vya Umeme nitumiavyo kutibu na kuremba Nywele zangu.



Nathamini na kuheshimu Muda wako hapa, ahsante sana kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Comments

Nanah said…
Bidhaa za aphogee protein 2 treatment zinapatikana wapi?

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao